Luke 7:18-23

18 aWanafunzi wa Yahya Mbatizaji wakamweleza Yahya mambo haya yote. Hivyo Yahya akawaita wanafunzi wake wawili 19 bna kuwatuma kwa Bwana ili kumuuliza, “Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?”

20Wale watu walipofika kwa Isa wakamwambia, “Yahya Mbatizaji ametutuma tukuulize, ‘Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?’ ”

21 cWakati huo huo, Isa aliwaponya wengi waliokuwa na magonjwa, maradhi na pepo wachafu, na pia akawafungua vipofu wengi macho wakapata kuona. 22 dHivyo akawajibu wale wajumbe, “Rudini mkamwambie Yahya yote mnayoyaona na kuyasikia: Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa habari njema. 23Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.”

Copyright information for SwhKC